
MUIGIZAJI Jussie Smollett aliyetambulika kama Jamal Lyon kwenye Empire Series amepatikana na hatia kwenye makosa matano kati ya sita ya utovu wa nidhamu kwa kutoa ripoti ya uwongo kwa polisi wa Chicago kwamba alikuwa mwathirika wa uhalifu wa chuki mnamo Januari 2019, ambapo waendesha mashtaka walisema aliigiza.
Jopo la majaji sita wa kiume na sita wanawake walijadili kwa zaidi ya saa tisa Jumatano na Alhamisi. Muda wote, Smollett, akiwa amevalia suti na tai, alionekana akitazama mbele, mikono ikiwa juu ya meza.
Ni kosa la jinai daraja la 4 ambalo linahusu kutoa ripoti ya uhalifu wa uwongo na adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka mitatu gerezani na faini ya dola za Marekani 25,000 (Tsh milioni 57.575).
Jaji wa Mahakama ya Kaunti ya Cook, James Linn atatoa hukumu baadaye ama kwa wakati mmoja au kila kosa na adhabu yake.