×

Nyashinski Afunga Ndoa

MWANAMUZIKI Nyamari Ongegu maarufu Nyashinski amefunga ndoa na mpenzi wake Zia Bett katika hafla ya faragha iliyofanyika mapema jana Desemba 10, 2021.

Nyota huyo alisindikizwa na mastaa kadhaa akiwamo aliyekuwa mshirika wake mkubwa kwenye bendi yake ya Kleptomaniax, Dj Stylez, Big Pin, pamoja na Wahu.

Huku nafasi ya mpambe wake ikishikiliwa na meneja wake wa zamani ambaye kwa sasa ni mtayarishaji wa Filamu maarufu nchini humo Fakii Liwali pamoja na msanii Nameless. Nyashinski na Zia Bett ni wapenzi wa muda mrefu na wamebarikiwa kupata mtoto mmoja.

Leave a Comment