×

Mkubwa Fella: Siyo Kama Hatuwaoni

MENEJA wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz. Said Fella Mkubwa Fella anasema kuwa, mara nyingi wao kama viongozi huwa wanawaona baadhi ya watu ambao wanamtukana msanii wao, lakini wanaamua kunyamaza.

Mkubwa Fella ameiambia IJUMAA SHOWBIZ kuwa, wana uwezo wa kuwachukulia hatua za kisheria, lakini wanawapuuzia kwa sababu mtu mwenye akili timamu hawezi kubishana na mpumbavu.

“Siyo kama hatuoni, huwa tunaona sana jinsi Diamond anavyotukanwa huko mitandaoni, wasidhani kuwa hatuoni, lakini tunakaa kimya kwa sababu hiyo ndiyo hulka yetu, siku zote wanasema kukaa kimya ni jibu la mjinga na hicho ndicho tunachokifanya.

“Hatuna muda wa kuwachukulia sheria, acha waendelee kuwa wapumbavu kwa sababu msanii wetu sisi anazidi kukua na kutoa burudani nzuri kwa mashabiki wake wanaomuweka mjini,” anasema Mkubwa na Wanawe.

STORI; MEMORISE RICHARD, DAR

Leave a Comment