×

Idd Nado Nje Miezi Sita

Daktari wa klabu ya Azam, Mwanandi Mwankemwa, amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Idd Seleman ‘Nado’, atakuwa nje ya dimba kwa muda wa miezi tisa akiuguza majeraha ya kukatika mtulinga wa kati (Anterior Cruciate Ligament) wa goti lake la mguu wa kulia.
Mwankemwa yupo jijini Cape Town, Afrika Kusini na nyota huyo, kwa ajili ya matibabu kwenye Hospitali ya Vincent Pallotti. Nado alipata jeraha hilo wakati Azam FC ikiichapa Mtibwa Sugar bao 1-0, Novemba 30, mwaka huu.

Leave a Comment