×

Vodacom Yaendelea Kushirikiana na Wadau Kuwaletea Wateja Huduma na Bidhaa Bora

Geoge Lugata

 

 

Akizungumza na wanahabari Mkuu wa Mauzo wa Vodacom George Lugata amesema Vodacom inayofuraha kubwa kuzindua huduma ya manunuzi ya simujanja kwa mkopo ambao Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na D. Light inaleta kwa wateja wake.

 

Kama mnavyofahamu matumizi ya simujanja yameongezeka kwa kasi nchini. Lakini licha ya ongezeko hili bado takriban theluthi mbili kati ya tano hawatumii simujanja, ambapo kwa kutumia simu hizo, ndipo mtu anapata huduma za intaneti.

 

 

Uzinduzi wa huduma hii umelenga kutatua changamoto kubwa inayorudisha nyuma matumizi ya simujanja ambayo ni bei ya kununua simu hizi.

 

Sasa wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC wanaweza kutembelea duka letu lolote nchini na kuwa na nafasi ya kupata mkopo wa simu za kijanja kwa kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa.

 

Pamoja na hayo, sisi Vodacom Tanzania Plc, hatujawasahau wateja wetu, kila atakayenunua simu hii atapata GB 96 kwa mwaka mzima, hii yote ni katika kuhakikisha kwamba hatuachi mtu nyuma.

 

Kwa kupitia ushirikiano huu, mteja wa Vodacom atakiwa kulipia Tsh 80,000 tu na ataondoka na simu yake, halafu atakuwa akilipia shilingi 1,800 kwa siku kwa muda wa siku 300 ili kumaliza deni analodaiwa.

 

Kukuza ujumuishwaji wa kidijitali tunataka kuhakikisha kila Mtanzania anapata simujanja na kama kampuni tumeandaa mikakati tofauti ili kufanikisha ongezeko la matumizi ya simujanja nchini, hii ni pamoja na kusambaza simu za bei rahisi kama smartkitochi ambayo inauzwa kwa TZS 38,000.

 

Lengo letu kuu ni kuwapa Watanzania wengi zaidi fursa ya kumiliki simujanja ili waweze kufaidika na huduma mbalimbali zinazopatikana kupitia mfumo wa kidijitali kama:

Huduma ya Vodacom Instant schools ambayo ni mfumo wa kupata maudhui mbalimbali zikiwemo taarifa za masomo kuanzia shule za msingi mpaka shule za sekondari.

Huduma ya Vodacom M-Kulima, sehemu ambapo watumiaji wanaweza kupata taarifa mbalimbali za Kilimo zikiwemo taarifa za masoko, pembejeo, hali ya hewa nk.

Huduma ya M-Pesa ambayo wateja wanaweza kutuma na kupokea pesa pamoja na kulipia matumizi mbalimbali kupitia mfumo wa M-Pesa. Na mengineyo mengi.

 

  • Napenda kuchukua nafasi hii kushukuru ushirikiano wa D. Light katika kuleta huduma hii ya mkopo wa simujanja kwa wateja wetu.

 

  • Ninatoa wito kwa wateja wote wa Vodacom kuchukua nafasi hii  katika msimu huu wa sikukuu kuhakikisha wanachukua fursa ya kupata au kumnunulia umpendaye simujanja ili afaidike na ulimwengu wa kidijitali wa leo.

Leave a Comment