
KLABU ys Simba imezindua rasmi Kampeni ya uchangiaji fedha ili kujenga uwanga wake ambao utagarimu zaidi ya Sh bilioni 30.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbra Gonzalez amesema kaulimbio yao kuelekea kwenye kampeni hiyo ni Simba yetu Uwanja wetu na ameomba wanachama na mashabiki wao kujitokeza kwa wingi kuchangia ili kutimiza ndoto zao.
“Namshukuru Mwenyekiti wetu mstaafu wa Bodi ya Wakurugenzi Mohamed dewji kwa kutuchangia Bil.2, sasa ni zamu ya mashabiki nao kutumia fursa hiyo kuweza kujitoa kwa ajili ya kufanikisha mchakato huo ili klabu ya Simba kuwa tofauti na nyingine hapa nchini,” amesemaBarbra.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa timu hiyo Murtaza Mangungu amesema uwanja huo utabeba watu elfu 30 na amesema wanatarajia kuzindua michoro ya uwanja huo mapema mwezi Januari.