×

Cardi B Amzawadia Offset Bilioni 4

Rapa machachari nchini Marekani, Cardi B amemzawadia mume wake, Offset zawadi ya dola milioni 2 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 4 za Kibongo katika hafla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika usiku wa Desemba 21, Los Angeles nchini humo.

 

Hili siyo jambo geni kwa wawili hawa, kwani wamekuwa wakipeana zawadi zenye thamani kubwa kwa miaka kadhaa.

 

Offset ambaye pia ni rapa, alimpa Cardi B zawadi ya nyumba yenye thamani ya dola milioni 1.5 za Kimarekani ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 3, Katika ‘birthday party’ yake ya kutimiza miaka 29 iliyofanyika Oktoba, mwaka huu.

 

Kupitia Instagram katika Instastory ya Cardi B, ameweka video ikimuonesha akiwa na check ya dola milioni 2 huku akipost picha ya kumtakia maisha marefu mume wake huyo katika siku yake ya kuzaliwa.

 

Zawadi kubwa kuwahi kupewa au kumpa mpenzi/mume/mke wako ni ipi?

Cc; @bakarimahundu

 

Leave a Comment