Mkuu wa Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Birgita Shirima akizungumza kwenye hafla ya ugawaji zawadi hizo.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom imegawa zawadi mbalimabli kwa wateja wake walioshiriki kampeni yao ya ‘Show Love’ Tule Shangwe katika hafla iliyofanyika Soko la Tabata Muslim Dar.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Brigita Shirima amesema lengo la afya hiyo ni kugawa zawadi mbalimbali kwa ajili ya wateja wao waliojishindia kwenye kampeni yao ya ‘Show Love’ Tule Shangwe.

“Tulianza kampeni hii zaidi ya wiki tatu zilizopita sasa na leo tumekuja kugawa zawadi mbalimbali kwa washindi wa kampeni ambapo miongoni mwa zawadi walizojishindia ni pamoja na Tv, Smart Phone, Pesa Taslimu na zawadi nyinginezo”, alisema Brigita.
Brigita amesema jinsi ya kujishindia kwenye kampeni ni kuwa mtumiaji wa Vodacom na kubonyeza *149*01# nunua bando hapo utakuwa umejiweka katika nafasi ya kushinda.
Amesema baada ya kufanya hivyo rudia tena kwenye menyu hiyo ingia namba 5 kwa ajili ya kuweka namba ya umpendae ili muweze kushinda wote.
Birgita amesema pia ukifanya huduma mbalimbali kupitia menyu ya M-Pesa na M-Pesa App nayo unajiongezea nafasi ya ushindi hivyo ni wakati wa watumiaji wa simu za mkononi kutumia huduma za Vodacom na kuweza kujishindia zawadi hizo, alimaliza kusema Birgita.
Hafla ilihudhuriwa na umati mkubwa uliofika eneo hilo kushuhudia washindi hao wakikabidhiwa zawadi zao.