
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Aitel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel TUNAKUJALI imetangaza kuzindua mpango kampeni maalum ili kuendeleza jitihada zake za kusaidia jamii kwa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ambapo inalenga kuwanufaisha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Kampeni itajulikana kama ‘Tabasamu na Aitel TUNAKUJALI’ kupitia kampeni hiyo itanufaisha mikoa 12 kwa kugusa vituo 12 vinavyolea watoto ili kuwapa tabasamu kwa kipindi hiki cha sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya.

Akizungumza Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kuzindua kampeni hiyo ya ‘Tabasamu na Airtel TUNAKUJALI’ Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano alisema;

“Katika kipindi hiki cha sikukuu tendo hili ni njia yetu ya kuonyesha upendo kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, tumewiwa kuwafanya watabasamu kuwaonesha tunawajali na kuwapa matumaini ya baadae.
“Kwa msimu huu tunawapa kidogo kwa upendo ili na wao waweze kusherehekea sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.
“Tutatoa msaada kwa vituo 12 vya watoto vilivyopo katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma, Lindi, Kagera, Mtwara, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya.
Singano aliongeza, “Furaha ya Airtel siku zote imekuwa ni sababu ya kubadilisha maisha ya wengine kupitia miradi mbalimbali kama Airtel TUNAKUJALI Tunaamini katika dhana ya jamii iliyo sawa na ndiyo sababu tumechagua msimu wa sikukuu kuishi na watoto hawa” alisema Singano.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Godwin Gondwe ambaye alizindua kampeni hiyo ya ‘Tabasamu na Airtel TUNAKUJALI’ aliwapongeza Airtel kwa kuwasaidia watoto hao hasa kwa kuwakumbuka kwa kipindi hiki cha msimu huu wa sikukuu.
“Natambua kuwa Kampuni ya Airtel Tanzania inamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 49 na nina uhakika chini ya umiliki mpya Airtel itaendelea sio kuwekeza tu kwenye masuala ya kusaidia jamii peke yake lakini pia upanuzi wa mtandao kitu ambacho ni lazima tukipongeze,” Gondwe alisema.
“Nimepewa taarifa kuwa Airtel kwenye kusaidia jamii imeshirikiana na serikali kwenye ujenzi wa Hospitali Uhuru jijini Dodoma kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni mbili.
Ujenzi wa hospitali bado unaendelea na ukikamilika itakuwa ni moja ya hospitali kubwa na yakisasa kwenye ukanda huo.
Bado naendelea kushuhudia Airtel ikiendelea kurudisha kwa kusaidia jamii mnayoihudumia ,leo hii nashuhudia ‘Tabasamu na Airtel TUNAKUJALI’ ambayo imekuja wakati muafaka ambapo marafiki na wanafamilia wakisherehekea na watoto wetu hawa watasherehekea pia.
Nawapongeza sana na nawaomba muendelee kusaidia jamii haswa watoto kama hawa wanaoishi kwenye maingira magumu”, Gondwe alisema.
Naye kiongozi wa kituo cha watoto hao kiitwacho Ijango kilichopo kilichopo Sinza, Dar baada ya kupokea msaada huo aliishukuru Airtel kwa msaada huo ambao umewafikia wakati muafaka yaani kipindi hiki cha sikukuu ambapo watoto hao nao sasa watasherehekea sikukuu kama watoto wengine.
Mlezi huyo wa watoto hao aliiomba Airtel kuendelea misaada kama hiyo na kwenda kuwasaidia na wengine wenye uhitaji kama wao na kuziomba taasisi zingine na watu binafsi kuwa na moyo kama huo.
HABABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL