
Proucer maarufu duniani, Andre Romelle Young ‘Dr Dre’ (56) wamefikia makubaliano rasmi ya kuvunja ndoa yake na aliyekuwa mke wake Nicole Young japokuwa itamgharimu Dre kiasi cha dola milioni 100 za Kimarekani ambazo ni sawa na Tsh bilioni 230 kuvunja ndoa hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa TMZ, Dre pamoja na mke wake wamefikia makubaliano hayo baada ya kudumu katika ndoa yao kwa takribani miaka 25 na kuachana rasmi kisheria kutokana na tofauti zilizojitokeza baina yao.
Nicole atapokea dola milioni 50 kwa sasa, na nyongeza ya dola milioni 50 ndani ya mwaka mmoja, ambayo ni sawa na malipo ya $ 100 milioni kwa jumla.
Dre na Nicole walioana mwaka 1996 na kufanikiwa kupata watoto wawili, wa kike Truly Young, 20, na wa kiume Truice Young, 24 na hivi karibuni baada ya kuachana, jamaa huyo alifanya sherehe kusherehekea talaka yake na Nicole.
Wawili hao wamekuwa kwenye ugomvi kwa muda mrefu na kuiomba mahakama kuvunja ndoa yao huku Nicole akidai kuwa amekuwa akinyanyaswa na mumewe huyo kwa kushushiwa kipigo na kutishiwa kuuawa mara kadhaa kwa kuwekewa bastola kichwani.
Aliongeza pia kuwa Dre alimfukuza Nicole ndani ya nyumba yao na kumfanyia vitendo vya udharirishaji wakati msanii huyo akiwa amelewa tungi lakini rapa huyo alikana kuwa hajawahi kumfanyia vitendo hivyo vya unyanyasaji.