×

Babu Tale: Bila Mke ni Mtihani

Maneja wa Diamond Platnumz ambaye pia ni Mbunge Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Taletale ‘Babu Tale’ amefunguka tena kwa mara nyingine kuhusu umuhimu wa mkewe alipokuwepo enzi za uhai wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Babu Tale ambaye alimpoteza mkewe jana 2020, ameandika.

 

“Siku tatu zijazo yaani tarehe 31/12/2021, naenda kutimiza miaka 40 kwa uwezo wake Mola inshallah. Ila kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu nitaitimiza miaka 40 bila mke, lakini nina watoto wanne (4).

 

“Uzee bila Mwenza ni mtihani ila bado nasubiri wakati wa Mungu ufike ndipo nitakapo fanya maamuzi. Kuhusu majiamoto bafuni nitaweka hita au jiko la mkaa.

 

“Asante Mungu kwa kuendelea kunilinda na kunipa uimara, naomba uendelee kunipa nguvu ya kulitumikia jimbo letu la Morogoro Kusini Mashariki na kulilinda kwa mikono yako, maana matarajio ya kazi nitakazozifanya Mwaka ujao, Mungu pekee ndiye anajua inshallah. Mungu awabariki. Naanza kupokea zawadi ndugu zangu,” ✍️@babutale.

Leave a Comment