×

Man United Yachezea Kichapo Nyumbani

Manchester United imekubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Wolves katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Old Trafford, Jumatatu Januari 3, 2022.

 

Bao pekee likifungwa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Joao Moutinho akipiga shuti la chini chini akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea mpira uliokuwa umeokolewa na beki Phil Jones dakika nane kabla ya kumalizika kwa mtanange hupo.

 

Kipigo hicho kinahitimisha utawala wa kutopoteza mechi yoyote kwa kocha Ralf Rangnick ambaye kabla ya mchezo huo alikuwa hajapoteza.

 

Matokeo hayo yanaifanya Wolves wanabakia nafasi moja nyuma ya Manchester United wakati United wakiwa alama 22 pungufu ya vinara Manchester City wakiwa na alama 31.

 

Ushindi huo wa Wolves ndani ya Old Trafford unawafanya kuandika rekodi mpya baada ya kupita miaka 42 pasipo kupata ushindi katika uwanja huo.

Leave a Comment