
STAA wa muziki nchini Marekani, Jason Derulo amepambana kwa kupigana na watu wawili katika hoteli ya ARIA huko mjini Las Vegas kwa madai ya kwamba wamemuita jina la msanii wa R&B ‘Usher’.
Kutokana na habari zilizochapishwa na mtandao wa TMZ, polisi waliitwa kwenye hoteli hiyo asubuhi ya jana Jumanne Desemba 4, 2022 baada ya Derulo kuwarushia ngumi wanaume hao kwa kumuita ‘Usher’.
Aidha, watu walioshuhudia tukio hilo wamrdai kwamba Derulo na jamaa hao walikuwa wakipishana kwenye ngazi, ndipo mmoja wao alionekana kumpapasa Derulo huku akipiga kelele, “Hey, Usher! huku akitamka maneno mengine yasiyo mazuri, jambo ambalo lilimchukiza Derulo.
Alimtwanga moja kwa moja ngumi ya uso na jamaa yule kuanguka chini huku akimtwanga kofi mtu wa pili kabla ya askari wa usalama kuingilia kati kuzuia ugomvi huo.
Imeelezwa kwamba, jamaa hao walioshambuliwa hawakutaka kushtaki kwenye vyombo vya dola lakini kwa mujibu wa sheria wana hadi mwaka mmoja wa kuamua kubadili mawazo yao ikiwa wataamua kumpeleka Derulo mahakamani au kupuuzia jambo hilo.