
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Albert Chalamila amekanusha taarifa iliyosambaa mtandoni ikionyesha kuwa ameunga mkono mabadiliko ya katiba jambo ambalo amesema amelishwa maneno na kwamba yeye si muumini wa mlengo huo huku akisisitiza msimamo wake alionao.
Chalamila amesema hataki katiba mpya wala marekebisho yake na kwamba habari zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba anaunga mkono mabadiliko ya katiba ni za uongo hivyo zipuuzwe.
“Wala sihitaji hiyo katiba mpya, wala sihitaji hayo marekebisho,” amesema Chalamila.