
IKIWA ni takriban miaka minne ya ujenzi, barabara ndefu zaidi ya chini ya maji nchini China, hatimaye barabara hiyo imeanza kutumika kwa kupitisha magari chini ya Maji ya katika Ziwa Taihu.
Barabara hiyo ina na urefu wa kilomita 10.79 (sawa na maili 6.65) ikiwa imejengwa kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 1.56 (sawa na Tsh trilioni 3.583).
Zaidi ya mita za ujazo milioni 2 za saruji zilitumiwa kujenga handaki hili lenye njia sita na upana wa mita 17.45 likiwa limenakshiwa na taa za rangi za LED ambazo pia zinatajwa kusaidia kumuondolea Dereva uchovu.
Barabara hii ya chini ya ziwa ni sehemu ya Barabara kuu ya Changzhou-Wuxi yenye urefu wa kilomita 43.9 ambayo ilianza kutumika tarehe 30 Desemba 2021 ikitoa mbadala wa haraka kwa Wasafiri wanaosafiri kati ya Shanghai na Nanjing, mji mkuu wa Jiangsu.