×

Airtel Wape Tabasamu Yafaidisha Tena Vituo vya Watoto Yatima Mikoa Mitano Wiki Hii

Meneja wa Mauzo Kanda ya Kati kampuni ya simu ya Airtel, Salumu Ngururu (kulia) akimkabidhi mwanafunzi wa shule ya msingi Hombolo Bwawani, Gwelina Mandama msaada wa vitu mbalimbali vilivyo tolewa na Airtel Tanzania kupitia kampeini ya wape Tabasamu mwishoni mwa wiki. Msaada huo ni pamoja na sukari, unga wa ngano, sabuni na mafuta ya kupikia.

 

 

 

KAMPENI maalum ya kusaidia jamii na hasa kwa kipindi hiki cha msimu wa sikukuuu ambayo inalenga kuwanufaisha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ya Airtel wape tabasamu imefikia mikoa mingine mitano mwishoni mwa wiki. Kampeini hiyo ya wafanye watabasamu, ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka jana mwishoni mwa wiki hii imeweza kufikia mikoa ya Mtwara, Lindi, Dodoma, Singida na Kigoma.

Ikiwa chini ya mwamvuli wa TUNAKUJALI, wape tabasamu imeweza kufikia vituo vya watoto yatima vya Assemblies of God (TAG) mkoani Mtwara, Naweza Mkoani Lindi, Hombolo mkoani Dodoma, Ititi mkoani Singida na Brothers of Charity mkoani Kigoma.

Akikabidhi msaada kwa kituo cha Brothers of Charity mkoani Kigoma, Meneja Mauzo Airtel Kanda ya Kigoma Gibson Fwankiye alisema kuwa kampuni ya Airtel kwa muda mrefu imekuwa ikisaidia jamii na sana sana kwa watu wenye uhitaji maalum kwa lengo la faraja.

 

Meneja wa mauzo Airtel Tanzania Kanda ya Singida na Manyara Kephar Jason (kushoto) akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe. Yagi Kiaratu ili kukabidhi kwa uongozi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Ititi cha Singida mjini vilivyo tolewa na Airtel Tanzania kupitia kampeini ya wape Tabasamu mwishoni mwa wiki. Msaada huo ni pamoja na sukari, unga wa ngano, sabuni na mafuta ya kupikia.

 

 

 

‘Hatua hii ni moja ya kusema asante kwa Watanzania kwa kuendelea kutuamini na kutumia wetu. Vile vile, ni kurundisha sehemu ya faida yetu kwa jamii ambayo imekuwa ni watu muhimu sana kwenye biashara yetu. Naomba mpokee hiki kidogo tuliokuja nacho na sisi Airtel na hasa kwa Kanda hii ya Kigoma tutaendelea kuja kuwatembelea pamoja na kuwapa faraja kwa watoto hawa’ Fwankiye alisema.

Mgeni maluum kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo ambaye ni Diwani wa Kata ya Bangwe iliyopo mjini Kigoma Khamis Betese, amewapongeza Airtel kwa kuwakumbuka watoto wenye uhitaji maalum na kuja kutoa msaada wa chakula. ‘Nawapongeza kampuni ya Airtel kwa kuwajali wenye uhitaji maalum na leo tuko pamoja kwenye kituo hiki cha Brothers of Charity. Nawaomba isiwe mwisho wa kuja kwenu hapa na sisi tutaendelea kuwaunga mkono kwenye biashara zenu,’ alisema Betese.

Aidha Mratibu wa Kituo cha kulelea Watoto wenye Ulemavu cha Brothers of Charity Jonas Kavunyi amesema watoto wenye ulemavu wameongezeka zaidi katika kituo hicho na kwamba uhitaji ni mkubwa wa mahitaji kwa watoto hao, na kwamba hakuna gharama zozote zinazohusisha watoto hao ambapo ametoa wito kwa jamii na mashirika kuguswa na kusaidia wahitaji.

Ameongeza kuwa kutokana na Kampuni ya Airtel kurudisha fadhira kwa jamii amewaomba watanzania kuendelea kutumia mtandao huo na kuchochea hamasa ya mtandao huo kusaidia jamii.

‘Tunawashukuru na kuwapongeza Airtel kwa kuguzwa kwao na kuja kutupa msaada huu. Kituo chetu kina mahitaji mengi na sisi tunatengemea wafadhili kukiendesha. Tunawaambia karibuni tena na tunahidi kuwa tutakuwa mabalozi wema wa kampuni yenu,’ alisema Kavunyi.

Leave a Comment