
NYOTA wa mitandao ya kijamii na televisheni Kim Kardashian ni miongoni mwa watu watatu maarufu waliotajwa katika mashitaka yanayoendelea ya watu waliowekeza pesa zao katika Kampuni ya sarafu za kidigitali inayofahamika kama Itrium Max Cryptocurrency na kupoteza pesa zao.
Watu wengine wanaoshitaki ni pamoja na mwanandondi Floyd Mayweather Jr., mchezaji wa mpira wa kikapu, Paul Pierce na wabunifu wa mfumo wa malipo ya pesa za kidigitali – cryptocurrency.
Nyaraka za kesi hiyo zinadai kwamba watu maarufu walishirikiana na Idrium Max “kuwawakilisha kimakosa na kuuza pesa zao za kidigitali” lakini Itriyam Max ilikana madai hayo.
Idrium Max Cryptocurrency imesema haina uhusiano wowote wa kisheria au kibiashara na pesa zilizouzwa katika mfumo wa pesa za kidigitali chini ya jina Ethereum, hivyo kesi bado inaendelea.