
VISA vya ajali za moto kuteketeza majengo jijini Dar es Salaam vimezidi kuendelea ambapo leo, Alhamis, Kikosi cha Zimamoto kimembana kudhibiti moto uliotekea katika jengo la ghorofa nane mtaa wa Lumumba hatua chache tu kutoka soko la kariakoo lililoteketea kwa moto mwaka jana.
Jengo hilo linalotumika kwa makazi na biashara liliungua sehemu ya juu na baadhi ya maeneo kwa chini hata hivyo hapakuwa na majeruhi wala kifo katika ajali hiyo iliyotokea mapema asubuhi.
Ikumbukwe kuwa Usiku wa kuamkia Jumapili soko la wafanyabiashara wadogo machinga lililopo Karume jijini Dar es Salaam nalo liliteketea kwa moto na mamlaka bado zinaendelea na uchunguzi.