
Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Suzan William Mkangwa kuwa Kamishna wa Kazi, akichukua nafasi ya Brigedia Jenerali Francis Mbindi aliyepangiwa majukumu mengine.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffer Haniu, uteuzi huo umeanza Januari 17, 2022 ambapo kabla ya kuteuliwa katika nafasi hiyo, Mkangwa alikuwa mtumishi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.