×

Tuzo za Grammy Zarejea Tena

HATIMAYE zile Tuzo kubvwa duniani za Grammy 2022 zimerejea tena baada ya kusitishwa kwa muda kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuepuka kuenea kwa Covid-19.

CBS na Recording Academy wametangaza kuwa tukio la utolewaji wa tuzo hizo litafanyika huko Las Vegas nchini Marekani siku ya Jumapili, April 3.

Tuzo za Grammy hapo awali ilikuwa zifanyike Crypto.com Arena iliyopo Los Angeles Januari 31, lakini iliahirishwa kutokana na sababu zilizotajwa kuwa ni kuepuka hatari ya maambuki ya virusi vya Covid-19 kutokana na kuripotiwa kwa visa vipya kadhaa nchini humo kadhaa.

Mkurugenzi mtendaji wa Recording Acardemy Harvey Mason Jr. Akiongea na CNN alisema “Tunafuraha kuipeleka hafla ya tuzo za Grammy Las Vegas kwa mara ya kwanza, na kuifanya kwa ukubwa wa viwango vya dunia.”

Trevor Noah, mchekeshaji na mtangazaji maarufu wa kipindi cha “The Daily Show” ametangazwa kuwa mshereheshaji mkuu wa hafla hiyo kwa mara nyingine tena.

Leave a Comment