×

Vic Mensa Anaswa na Mihadarati Marekani

HIT maker wa ngoma ya ‘You Mad’ rapa Vic Mensa amekamatwa kwa kosa la kujaribu kuingia nchini Marekani na mihadarati aina ya ‘Shrooms‘ ambayo kwa majina maarufu huitwa Psilocybin Mushrooms au ‘Magic Mushrooms’ akitokea nchini Ghana.

 

Kwa mujibu wa sheria za nchi hio ni kosa la jinai kukutwa na majani hayo ambayo alikamatwa nayo Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles nje kidogo na Washington, D.C.

 

F.B.I Bado wanachunguza madhara halisi ya dawa hizo huku pakiwa na kampeni kubwa nchini Marekani kuruhusu matumizi ya ‘Shrooms‘ kuwa ruksa baada ya watu kudai hutumia majani hayo kama sehemu ya dawa na imani zao.

 

Vic Mensa alikuwa nchini Ghana pamoja na msanii mwenzake Chance The Rapper ambapo kwa pamoja walipata nafasi ya kukutana na Rais wa nchi hiyo, Akufo-Addo pamoja na wasanii mbalimbali wazawa wa Ghana.

Leave a Comment