
TAARIFA kutoka Gazeti la The Sun inasema kuwa bondia mkongwe na mashuhuri duniani Mike Tyson (55) yuko katika hatua za mwisho za makubaliano ya pambano la maonyesho na sio mkanda dhidi ya staa wa mitandao ya kijamii Jake Paul (25).
Kwenye dili hili Tyson anaangaliwa kutengeneza zaidi ya dola milioni 30 baada ya pambano na kijana huyo, Jake ambaye tofauti ya umri wake na Tyson ni miaka 30.
“Mpaka sasa wameongea tu na kukubaliana, wanachosubiri ni mikataba kuandika, mgawanyo wa pesa, Mike anataka uhakika wa kiasi flani kabla ya pambano,’ limesema The Sun.
Hii itakuwa hatua kubwa kwa Jake ambayo anataka kukuza jina lake kwenye ulimwengu wa mchezo wa Boxing kwa kuingia ulingoni na bondia aliyewahi kuitwa ‘Bondia Hatari Zaidi Duniani’.