
MSANII nguli wa muziki duniani kutoka pande za Senegal, Akon anadaiwa mkwanja na aliyekuwa mshirika mwenzake (business partner) Devyne Stephens kiasi cha dola za Kimarekani milioni 4 (sawa na takribani Tsh bilioni 9.2).
Imeelezwa kwamba Devyne anadai dola za Kimarekani 750,000 pamoja na dola za Kimarekani milioni 3 za mirabaha.
Kama sehemu ya masharti ya makubaliano yao ya mkataba wao wa kibiashara mwaka 2018, Akon alikubali kumlipa Stephens dola milioni 3.25 katika kipindi cha miaka minne lakini bado hajalipa awamu ya mwisho ya kiasi cha dola 750,000 kwa mijibu wa mtandao wa Pagesix.