Wekundu wa Misimbazi Simba leo Januari 22, imeshindwa kutamba mbele ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Manungu Turiani Morogoro.

Mashabiki wa soka leo wameshindwa kupata burufani ya baada ya uwanja wa Manungu kujaa maji kutokana na mvua kunyesha hivyo timu zote kudhindwa kandanda safi.
Mwamba wa Lusaka Clatous Chama alicheza mechi ya kwanza tangu arejee kwenye Simba na kuingia kwake kulibadilisha mchezo kwa Simba na kuanza kufika mara kwa mara kwenye langu la Mtibwa Sugar.

Simba sasa inafikisha alama 25 baada ya kucheza michezo 12 na mahasimu wao Yanga wanaendelea kubaki kileleni na pointi 32, kesho itashuka dimbani dhidi ya Polis Tanzania.