×

Miili ya Wasichana Ndugu Waliouawa Mwanza Yazikwa Sengerema

MIILI ya wasichana watatu wa familia moja waliouawa jijini Mwanza Januari 18, 2022 imewasilia mjini Sengerema na kuzikwa jana usiku Januari 21, 2022.

 

Waliokufa ni Mary Charles, Janeth Fred pamoja na Monica Jonas na miili yao ilipowasili wananchi waliangua vilio kutokana na mauaji yaliyofanywa na watu wasiojulikana.

 

Mmoja wa wakazi wa mtaa wa Bomani mjini humo Samson John amesema walikuwa hawajawahi kuchimba makaburi matatu na kuzika miili kwa wakati mmoja na kuiomba Serikali kuwabaini na kuwachukulia hatua waliofanya mauaji hayo.

 

Akiongoza ibada ya maziko nyumbani kwa marehemu Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Imakulata Bomani mjini humo, Padri Fred Mgabi amesema waliofanya mauaji hayo hawana hofu ya Mungu na hawajawahi kufika kanisani.

 

Amesema huku ya watu waliyotekeleza mauwaji haya hukumu yao wataikuta kwa Mungu kutoka na matendo Yao. Baadhi ya wakazi wa mjini wa Sengerema wameiomba Serikali kuchunguza tukio hili na kuwachukulia hatua watu waliyotekeleza mauaji haya Ili liwe fundisho kwa watu wengine.

Leave a Comment