
MWANAMUZIKI maarufu nchini Harmonize ameendelea kuonesha heshima kwa mwanamuziki mwenzake Ali Saleh Kiba kwa kumpongeza kwa kazi nzuri kupitia kwenye moja ya post zake aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (insta story).
“Mtu amwambie mkongwe, mfalme Ali Kiba lazima aimbe kwenye usiku wa kumvisha pete mchumba wangu, huu muziki mzuri sana,” amesema Harmonize.
Harmonize ameandika maneno hayo huku akiambatanisha na kipande kidogo cha video akisikiliza wimbo ‘Utu’ wa msanii Ali Kiba.