
MWANAMAMA wa Bongo Movies, Kajala Masanja au Frida Kajala amemuonya msanii wa nyimbo za Injili nchini Kenya, Ringtone kuwa aache kumtumia jumbe mbalimbali.
Kwa mujibu wa Kajala, Ringtone amekuwa akimtumia jumbe mbalimbali yeye pamoja na mwanawe, Paula Kajala.
“Nikome kunitumia messages na kumtumia mwanangu Paula Kajala. Wanaume wa Kenya sijui ni nini mbaya na nyinyi,” aliandika Kajala akiuelekeza ujumbe wake huo kwa Ringtone.
Hii sio mara ya kwanza Ringtone kuwatamani watu maarufu wenzake, lakini wamekuwa wakimkataa.