×

Barbara: Ubingwa Ni Mali ya Simba Msimu Huu

MTENDAJI wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez, amesisitiza kuwa ishu ya nani atakuwa bingwa wa ligi kuu msimu huu, ipo wazi ya kwamba Simba ndiyo watachukua tena kombe.

 

Barbara amefunguka kuwa, msimu huu wanakutana na changamoto nyingi ambazo anaamini zinatengenezwa makusudi ili kuwakwamisha Simba, ila wanataka kuonyesha watu kuwa Simba ni timu kubwa haswa
ambayo ikitaka jambo lake lazima
lifanikiwe.


Akizungumzia ugumu wa ligi
msimu huu, Barbara alikiri kuwepo kwa ushindani zaidi ya msimu uliopita, ila hiyo kwao haiwezi kuwa kikwazo cha kutaka kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa kwa mara ya tano mfululizo. Licha ya
upinzani na ugumu wanaokutana
nao kwenye kila kona ya uwanja na nje pia.

 

“Suala la Simba kuwa bingwa msimu huu lipo wazi kabisa na halina mjadala, Simba ndiyo itachukua ubingwa. Tunakutana na ugumu na changamoto kubwa lakini hatuwezi kushindwa kabisa.


“Tutapambana hadi mwisho
kuwapa furaha wapenzi na mashabiki wetu wa Simba, tunataka kuwaonyesha kuwa
Simba ni timu kubwa ambayo
inaweza kupambana kwenye mazingira yote yanayokuja mbele yetu,” alisema.

STORI: ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

Leave a Comment