×

‘Mama Tetema’ ya Rayvanny Yatikisa Billboard

NGOMA ya ‘Mama Tetema’ aliyoimba supastaa wa Bongo Fleva, Raymnond Mwakyusa ‘Rayvanny’ pamoja na nyota wa muziki kutoka nchini Colombia, Maluma umefanikiwa kuzama hadi nafasi ya kwanza kwenye chati za muziki za Billboard nchini Mexico.

“Mama Tetema” remix ya ngoma ya Rayvanny ‘Tetema’ aliyomshirikisha bosi wake, Diamond Platnumz, kabla ya kuingia makubaliano ya kuirudia na Maluma.

Ikumbukwe kuwa, usiku wa kuamkia Novemba 15, 2021 ‘Mama Tetema’ ilitengeneza historia mpya ya muziki wa Rayvanny na Tanzania kwa ujumla baada ya staa huyo kupanda jukwaa moja na Maluma kutumbuiza kwenye hafla za utoaji tuzo za MTVEma.

Rayvanny aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kutumbuiza katika tuzo hizo kubwa duniani zilizofanyika László Papp Budapest Sports Arena huko Budapest, nchini Hungary.

Leave a Comment