×

Tango Aibuka Bingwa John Walker Waitara Trophy

NYOTA wa mchezo wa gofu, Injinia Joseph Tango mwenye handicap 13, juzi Jumamosi alifanikiwa kuibuka mshindi wa jumla wa mashindano ya gofu ya John Walker Waitara baada ya kupiga mikwaju 68.

Mashindano hayo ya siku moja yalifanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo, ambapo mgeni rasmi wa kilele cha tukio hilo alikuwa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Damas Ndumbaro.

 

Mara baada ya kutangazwa kuwa msindi wa mashindano hayo, Injinia Tango alisema: “Nashukuru kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mashindano haya, nawashukuru waandaaji pamoja na washiriki wote ambao walionyesha ushindani mkubwa, lakini zaidi sana naishukuru timu yangu kwa sapoti yao.”

Naye Mgeni rasmi Waziri Ndumbaro akizungumza na gazeti hili alisema: “Kupitia Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imetuagiza kuhakikisha tunaongeza mazao ya utalii na sisi kama Wizara tuliuzindua mchezo wa gofu kama sehemu ya mazao ya Utalii, ni wazi unafanya vizuri, tunawapongeza na tutaendelea kuwasapoti.”

Kwa upande wa wachezaji wa kulipwa mshindi wa kwanza alikuwa ni, Frank Mwinuka aliyekuwa na gross 70, Mshindi wa pili, Fadhili Nkya aliyepata gross 73 na Abdallah Yusuph aliyekuwa na gross 75 alikuwa mshindi wa tatu.

Leave a Comment