×

Basi la Kidia One Lapata Ajali

TAARIFA zilizotufikia hivi punde ni kwamba, watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya busi la Kidia One linalofanya safari kati ya Arusha-Dar kupata ajali eneo la Kikatiti wilaya Arumeru mkoani Arusha.

 

Basi hilo ambalo lilikuwa linatoka Arusha kuelekea Dar es Salaam limepata ajali leo Jumatatu Januari 31, 2022.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema litatoa taarifa baadaye kuhusu chanzo cha ajali pamoja na madhara yaliyotokea kutokana na ajali hiyo. Hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza maisha kutokana na ajali hiyo.

 

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo, wameeleza kwamba sababu kubwa ya ajali hiyo ni hali ya hewa ambapo mvua zilikuwa zikinyesha huku kukiwa na ukungu uliosababisha barabara kutoonekana vizuri na kwamba basi hilo.

…..Endelea kufuatilia taarifa zetu….

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave a Comment