
Benki ya Absa Tanzania imeendelea kuimarika karika shughuli zake za kibiashara licha ya misukosuko kwenye soko iliyotokana na janga la COVID 19, ambalo liliikisa karibia sekta zote ya benki nayo ikiwemo, ikiibka baada ya janga hilo na kujipatia faida baada ya makato ya kodi ya asilimia 1875 katika mwaka wa fedha wa 2021, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Abdi Mohamed amebainisha.
“ Mwaka wa fedha wa 2021 ulikuwa mzuri kwa upande wa ufanisi wa utekelezaji wa shughuli za kifedha ikizingatiwa kuwa benki ya Absa iliripoti hasara ya TZS 532m mwaka 2020 na kujipatia faida baada ya makato ya kodi ya Tsh 9.4bn mwaka 2021” , alisema Abdi Mohamed jana.
“ Hasara iliyoripotiwa kwa mwaka 2020 ilitokana na athari hasi za janga la COVID-19 lililoathiri sekta nyingi za uchumi ambalo vilevile lilitikisa ufanisi wa utekelezji wa shughuli za biashara za benki ya Absa, hasa kwa kusababisha kushuka kwa mapato na kuongeza hasara zinazotokana na mikopo inayosuasua kulipwa.”
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, faida kabla ya kodi pia imekua kwa kiasi kikubwa cha asilimia 210 ikilinganishwa mwaka hadi mwaka kutoka Tsh 4bn mwaka jana hadi Tsh 13bn mwaka 2021, ongezeko lililochagizwa na kushuka kwa gharama za mikopo inayosuasua kwa asilimia 30, kushuka kwa gharama za uendeshaji kwa asilimia 8, wakati huohuo benki ikibakia imara kwenye uzalishaji wa mapato kwa kulinganisha mwaka hadi mwaka.
Abdi Mohamed alisema vilevile kuwa mapato halisi yanayotokana na riba ya benki yalikua kwa asilimia 2 mwaka 2021 licha ya kukua kwa mikopo inayochukuliwa na muda ambapo kukua huko kulitokea ,na kupungua kwa kiwango cha riba, ikizingatiwa kuwa benki imeendelea kuboresha bei za mikopo ili kuifanya iwe nafuu kwa wateja.
Mkurugenzi wa Fedha wa Absa, Obedi Laiser, alisema : “ Mwaka 2021 biashara nyingi zimepata ahueni ingawaje siyo kwa kiwango cha kuridhisha kutokana na janga la COVID19 mwaka 2020, na na benki iliripoti ukuaji wa mikopo ya wateja kwa asilimia 17 na ukuaji wa amana ulikua kwa asilimia 2.1 kwa mwaka uliotangulia ikiambatana na kupungua kwa gharama zinazotokana na mikopo inayosuasua kwa asilimia 30 kutokana na wakopaji wengi kuongeza ufanisi katika shughuli zao za kibiashara. Amana za wateja zilitegemewa kukua kwa kasi ya asilimia 11 mwaka huo lakini iliathiriwa na mabadiliko ya sheria zinazoongoza akaunti ya dhamana ya fedha zinazopitia simu za mkononi.”
Benki ya Absa iliripoti ukuaji wa mikopo ya wateja katika nyanja zote za utoaji wa huduma za mikopo, ikiwemo wateja binafsi, mikopo ya kibiashara na mikopo mikubwa ya makampuni, huku benki ikijizatiti katika kutekeleza mpango mkakati wa kuboresha bidhaa za kidijitali, kupanua wigo wa wateja kwa aina mbalimbali za mikopo na kushiriki kwa upana zaidi katika shighuli za kuunga mkono sekta ya uma, kwa mujibu wa Laiser.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Mwaka 2021, benki ya Absa ilipanua aina za bidhaa zake kwa njia ya ubunifu, ikiwemo kuzindua mafumo wa utoaji wa mikopo binafsi kwa njia ya simu za mkononi kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Tigo, ambayo imesaidia maelfu ya wateja kufikia huduma za kifedha kwa urahisi zaidi na hivyo kuboresha maisha na ustawi wao.
Laiser aliendelea kusema kuwa kwa mwaka huo wa fedha Absa ilizindua huduma ya mikopo kwa biashara ndogondogo, na kuboresha mrengo wake wa kufanikisha miamala ya kidijitali kwa biashara hizo ndogondogo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo za kuongeza wateja kwa kila aina ya mikopo na kuboresha utoaji wa huduma za kidijitali. Kushiriki kwa benki kwenye sekta ya uma kwa 2021 kuliongezeka kwa kiasi kikubwa ikiwa ni utekelezaji wa azma ya benki katika kuchangia kwa njia endelevu kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania, ambayo nayo yanashika kasi kila kukicha.
Kwa upande wa kupanuka kwa benki, mtaji wote wa benki ulikua kwa kiasi cha kuridhisha cha asilimia 8.3 kwa mlingano wa mwaka hadi mwaka, hasa kutokana na kuwa faida iliyozalishwa kwa mwaka huo iliwekezwa tena kwenye mtaji wa benki. Mtaji wote wa benki uliongezeka kwa kiasi cha Tsh 11bn, kitu ambacho kiliongeza raslimali za mtaji ambazo nazo ziliwekezwa kikamilifu katika kukuza uwezo wa benki wa kutoa mikopo ili kuhudumia wateja weo kwa ubora zaidi.
Benki ya Absa inaendeela kuwa na kiwango cha mtaji imara ambacho kipo juu zaidi ya kiwango cha mahitaji ya mtaji wa ndani kilichopangwa kisheria. Uwezo wa kidijitali wa benki unazidi kukua na kuboreka, hivyo kuvutia wateja wengi zaidi na vilevile kuchagiza matumizi kwa wateja waliopo, alisema Mkurugenzi huyo wa fedha Laiser.
Kwa mwaka wa fedha wa 2021, benki ya Absa ilipata tuzo mbalimbali za ubora uliotukuka za ndani ya nchi na za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Kadi Bora za Benki Tanzania ( iliyotolewa na jarida la Global Magazine), Benki Inayongoza kwa Ubunifu kwenye Bidhaa za Wateja Binafsi, Tuzo ya Tanzania ( iliyotolewa na Global Business Outlook), na Taasisi Bora ya Kifedha kwenye Matumizi ya TEHAMA iliyotolewa mwaka 2021 na Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Tanzania.