
ACHANA na Video Vixen anayeonekana kwenye video ya Utu ya Alikiba, kumbe ishu ni kwamba muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya ndiye aliyetakiwa kuwepo kwenye video ya wimbo huo.
Hayo yamesemwa na Director wa video hiyo Ivan. Ivan alisema alikuwa anatakiwa mwanamke ambaye atakuwa na uwezo wa kuigiza pia na ndipo akatafutwa Uwoya.
Kila kitu kilikwenda sawa awali, lakini baadaye Uwoya akasema hataweza kuwepo kwenye video hiyo kutokana na kubanwa na michongo yake mingine inayompa mpunga mwingi.

“Uwoya alikuwa amesetiwa kila kitu baada ya kukubali kuwepo kwenye video hiyo, ikatafutwa location na baada
ya kuwa kila kitu kipo tayari, Uwoya akasema atashindwa kutokea.
“Alidai kuwa ratibazake zimembana na haitawezekana kufanya ishu zote kwa wakati mmoja. Sasa ikabidi tumtafute Nana Dollz ambaye naye anajua kuigiza na amefanya vizuri,” Ivan aliliambia Championi.
Utu ya Alikiba ilitoka Januari 28 na hadi sasa ndiyo video inayoshika namba moja kwenye YouTube Trending.