
Wabunge wanne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wamechukua fomu za kuwania kugombea unaibu Spika, leo Febriari 5 jijini Dodoma.
Wabunge hao ni pamoja na Mussa Zungu (Ilala), Mhandisi Samwel Hhayuma Xaday (Hanang), David (Mufindi Kusini) Kihenzile na Dk Hamis Kigwangalah (Nzega Vijijini) waliochukua fomu katika ofisi za makao makuu jijini Dodoma.
Nafasi ya unaibu Spika imeachwa wazi na Dk Tulia Ackson aliyechaguliwa kuwa Spika wa Bunge baada ya aliyekuwa Spika, Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na shinikizo la wana CCM.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na CCM jana, uchukuaji wa fomu umeanza Februari 4 hadi 6 na Februari 7 sekretarieti ya chama hicho itachambua maombi hayo na kuishauri Kamati kuu ambayo nayo itachuja majina ya wagombea Februari 8 kabl aya kupigiwa kura Februari 10.