×

Kanye Ataka Maelezo Mwanaye Kuunganishwa TikTok

Bado rapa Kanye West anapitia wakati mgumu tangu atengane rasmi na mke wake Kim Kardashian kitendo kilichosababisha rapa huyo kuwa mbali na watoto wake.

Mapema leo Februari 4, 2022. rapa huyo ameonesha wazi kutoridhiswa na kitendo cha mtoto wake wa kwanza North West kuunganishwa kwenye mtandao maarufu Duniani wa ‘TikTok’.

Kanye West ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuomba ushauri kwa mashabiki kuhusu suala la Kim Kardashian kumuunganisha mtoto wake kwenye mtandao wa TikTok bila ridhaa yake kama baba wa mtoto huyo.

“Nahitaji kujua ni kipi napaswa kufanya Kuhusu mwanangu kuunganishwa kwenye mtandao wa Tiktok bila ridhaa yangu” ameandika Kanye West.

Leave a Comment