
Rais wa Senegal, Macky Sall ametangaza kuwa leo Jumatatu Februari 7, 2022 ni mapumziko kitaifa ili watu washerehekee ushindi wa timu ya taifa ya Senegal baada ya kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021.

Rais huyo ambae alifuatilia fainali akiwa nje ya nchi, ameahirisha pia safari yake nje ya nchi ili awakaribishe Mabingwa hao Ikulu ambapo nyota hao wa soka watarejea nchini kwao leo Jumatatu, Februari 7. “Tumeongoja ushindi huu kwa miaka 60,” amesema Rais Sall.
Senegal waliishinda Misri 4-2 kwa mikwaju ya penalti na kupata ushindi wao baada ya fainali kumalizika bila kufungana iliyofuatiwa na muda wa nyongeza.