×

Kylie, Travis Wapata Mtoto wa Pili

SUPASTAA wa shoo ya Kimataifa ya Keeping Up With The Kardashians na mfanyabiashara, ambaye ni mdogo wake na mwanamitindo maarufu, Kim Kardashian aitwaye Kylie Jenner na mpenzi wake ambaye ni rapa maarufu duniani Travis Scott, wamefanikiwa kupata mtoto wa pili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kylie mwenye umri wa miaka 24 jana Jumapili alitangaza mtoto wao huyo wa kiume amezaliwa Jumatano ya Februari 2, 2022 (wiki iliyopita) ambapo kwa mujibu wa mtandao wa #TMZ #Kylie pamoja na mtoto wanaendelea vizuri.

Ndugu, jamaa na marafiki zake ikiwemo familia nzima ya Kardashian wamemiminika kumpa pongezi mrembo huyo kwa kushusha mtoto wa pili ikiwa ni miaka minne tangu apate mtoto wake wa kwanza Stormi.

Leave a Comment