×

Rais Samia Atoa Maagizo Kukamilisha Mfumo wa Anwani za Makazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa Kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi leo Februari 08, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

 

“Wizara ya Ardhi ndiyo yenye mamlaka na ardhi. Natambua kwamba kupitia utekelezaji wa mfumo huu mmeanza kufanya mageuzi makubwa kwa kuwa na ramani za kidijitali. Kazi hiyo ikikamilika itatuletea mageuzi ya utendaji upande wa ardhi, ikiwemo kuondoa migogoro ya ardhi

 

Serikali imedhamiria kwa dhati kutekeleza mfumo huu wa Anuani za Makazi ili kurahisisha utambuzi wa wakazi na makazi na kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na anuani ya makazi anapoishi ili kuwezesha kuhudumiwa kwa urahisi

“Natoa wito kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuendelea kuwashirikisha wananchi wenyewe na kuhakikisha mradi huu muhimu wa Anuani za Makazi unawahudumia wananchi kwa ufanisi. Hii itawafanya kuwa mabalozi imara na walinzi wa mitaa na miundombinu yao

“Kukosekana kwa Postikodi ilikuwa inatutenganisha na dunia kwani masuala mengi ya taarifa za kidijitali zinahitaji Postikodi, hivyo ilitufanya kukosa baadhi ya huduma ulimwenguni kupitia mitandao, lakini mfumo huu utaondoa tatizo hilo.

 

“Mwaka huu zoezi la Sensa litafanyika kikamilifu kwani itakuwa ni Sensa ya Watu na Makazi. Hii itakuwa tofauti na miaka ya nyuma kidogo ambapo tumekuwa na Sensa ya watu pekee bila makazi yao. Anuani za Makazi zitarahisisha zoezi hili

“Nawapongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar pamoja na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa uratibu mzuri na kutambua umuhimu wa jitihada za pamoja katika mipango ya maendeleo ya nchi yetu, nataka nipate ripoti ya kila hatua, changamoto tuzishughulikie,” amesema Rais Samia.

 

Awali,Waziri wa Habari, Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa atahakikisha kila mwananchi anakuwa na Anwani ya makazi ifikapo mwezi Mei, 2022.

Leave a Comment