
TAYARI nchi imeshatikisika kutokana na ujio wa timu ya Everton ambayo kesho Alhamisi itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa michuano ya SportPesa Super Cup, Gor Mahia ya Kenya. Mchezo huo umeshakuwa gumzo kutokana na aina ya wachezaji wa Everton watakaoonekana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakiongozwa na straika wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney ambaye juzi alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Everton, timu imara kwa miaka mingi kwenye historia ya soka la England.
Pamoja na Rooney, Everton ina wachezaji wengi mastaa ambao watakuwa burudani na hamasa kubwa kwa mashabiki kesho, baadhi yao wakiwa ni kiungo Morgan Schneiderlin, beki Leighton Baines, beki Ashley Williams, beki Phil Jagielka, kiungo Ross Barkley, straika Kevin Mirallas, winga mfupi lakini mwenye kasi Aaron Lennon, kiungo wa zamani wa Manchester City, Gareth Barry na Mholanzi aliyetokea Everton, Davy Klaassen.
Angalia majina hayo. Utaona kwamba hiyo ni fursa kubwa kwa Watanzania. Watu ambao tulikuwa tukiwaona kwenye televisheni, sasa watakuwa maeneo ya Temeke wakicheza soka mbele ya Watanzania. Lazima tufurahie fursa hii na ni lazima tukiri kwamba SportPesa wamefanya jambo la maana kuandaa mtanange huu wa Everton na bingwa wa SportPesa Super Cup.
Hii ni fursa kwetu Watanzania kujifunza wanavyofanya wengine. Siyo kitu rahisi kumuona ‘live’ Rooney akicheza mpira kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ingekuwa vyema sana kama timu zetu kubwa za Tanzania zingepata nafasi ya kucheza dhidi ya Everton lakini kwa kuwa zimekosa nafasi hiyo, twendeni tukashuhudie burudani Taifa, tuone jinsi wenzetu wanavyofanya. Niwaombe Watanzania wajitokeze kwa wingi kushuhudia mchezo huo, hata kama wengine wapo mikoani, kwa wanaoweza ni vyema wa
kasafiri kutoka huko waliko waje Dar es Salaam kuushuhudia mchezo huo kwani kuna mengi ya kujifunza na hii ni fursa adimu ambayo inatokea mara chache sana. Wengine, unaweza kuzaliwa hadi kufa bila kuwahi kuonana na mchezaji kama Wayne Rooney. Zinapopatikana nafasi ni vizuri kuzitumia vyema.
N a a m i n i watakaopata nafasi ya kuingia Uwanja wa Taifa kesho, watapata burudani ya aina yake, na itakuwa ni raha ya ajabu uwanjani siku hiyo. Ushauri wangu mwingine ni kwa wachezaji. Wadogo zangu hawa mechi hii ndiyo ya kwao, kwa lengo la kujifunza. Wachezaji wanaocheza kwenye Ligi Kuu Bara na ligi nyingine za chini, watumie fursa hii kwenda uwanjani kujifunza. Wanapoenda Uwanja
wa Taifa, wasiende kwa lengo la kuangalia mechi, badala yake waende kwa lengo la kujifunza. Uzuri bei iliyowekwa, kila Mtanzania anaweza kuimudu, kwa hiyo watu wajitokeze kwa wingi. Kwa mchezaji, anapaswa kuiangalia mechi hiyo kwa jicho la tatu. Mfano, mshambuliaji a n a takiwa aangalie Rooney anavyof a n y a a k i w a kwenye eneo la hatari. N a f a s i a n a zozipata anazitum i a j e , na tabia anayoionyesha kwa ujumla akifika katika eneo la hatari. Kutakuwa na vitu vingi vya kujifunza, ikiwa mchezaji ataitazama mechi hiyo kwa jicho la tatu. Hiyo ni fursa kubwa kwa mastaa wetu kujifunza mambo mbalimbali. Hata mabeki, wanatakiwa
kujifunza kwa beki kama Ashley Williams ambaye ni raia wa Wales aliyefanya mambo makubwa akiwa na timu ya taifa hilo kwenye michuano ya Kombe la Ulaya (Euro) kwa kuiwezesha kumaliza ndani ya nne bora, pia kazi yake inajulikana tangu alipokuwa Swansea. Kwa ujumla, kwa wachezaji wote wale, kuna mengi ya kujifunza kama wachezaji na kama Watanzania, hata makocha pia wanatakiwa wajitokeze wajifunze mengi katika mchezo ule. Kocha Ronald Koemann ana heshima kubwa katika soka la England kuanzia alipokuwa akiifundisha Southampton. Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona aliyewahi kuiwezesha Barca kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) mara nne mfululizo kuanzia 1991, 1992, 1993 na 1994 atakuwa na vitu vingi vya kuwapa Watanzania, akiwa kwenye benchi la ufundi la Everton. Hii si burudani ya kukosa kwa wapenzi wa soka. Kama kweli unapenda mpira, hauwezi kuikosa burudani hii bila kuwa na sababu ya msingi.
Mohammed Hussein