×

Kusah: Ruby Aangalie Sana

MSANII maarufu wa Bongo Fleva, Kusah unaambiwa hapoi, sasa ameamua kufunga ukurasa na mzazi mwenzake, Ruby ambaye amekuwa akimponda mitandaoni kila leo.

 

Akihojiwa na moja ya chombo cha habari hapa nchini, Kusah amesema kwa upande wake ameamua kumuachia mungu tu maana akiongea huenda akaharibu au vinginenvyo.

Kusah amesema; “Mimi sina mengi ya kuongea kwasababu sio mara ya kwanza kwake kuongea maneno hayo na vingi vipo vishaongelewa na huyo mtu tushamalizana ni mwaka wa pili sasa lakini tumebahatika kupata mtoto, kwa hiyo sisi ni wazazi hivyo ukiona mtu anathubutu kuandika vitu vile haileti maana hivyo sitamani hata kujibu.

“Huwezi jua nitajibu katika hali gani na itapokelewa vipi na watu kwaiyo ni sawa tu sababu Ruby ameanza kuongea muda na ameongea sana mimi namuachia yeye na Mungu wake, ila ajue kwamba ukweli unadumu na hii ni dunia kwa hiyo vitu vingine sio lazima uvifanye, aangalie sana. Ishu ya kumpeleka #Ruby kwa mganga yeye ndio kasema kwa hiyo hata mkimuuliza yeye itakua ni kitu kizuri zaidi,” amesema Kusah.

Leave a Comment