×

Simba Yashtukia Janja Ya Asec, Yatangaza Vita

LICHA yawapinzani waSimba, Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast kuficha kuhusu ujio wao hapa nchini
kwenye mechi ya kwanza
ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, wawakilishi hao wamesema
wala hawatishiki kwani
kichapo kipo palepale.

 

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao
utapigwa Jumapili hii kwenye
Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.


Simba ipo Kundi D, ikiwa
imepangwa pamoja na US Gendarmerie ya Niger na RS Berkane ya nchini Morocco
ambayo anaichezea Tuisila
Kisinda.


Akizungumza na
Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa maandalizi ya kikosi chao yamekamilika, ambacho jana jioni kiliingia kambini sambamba na kuanza mazoezi ya pamoja kuelekea mchezo huo.


Ally alisema kuwa, hadi
hivi sasa bado wapinzani wao hawajawapa taarifa za siku za kutua nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo mgumu ambao ni muhimu wapate ushindi nyumbani.

 

Aliongeza kuwa licha ya wao kutopata taarifa ya siku ya kutua nchini, wanaendelea na maandalizi ya nguvu kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya kushinda michezo yote ya nyumbani.

 

“Sisi kwa upande wetu Simba, tupo katika maandalizi mazuri ya mchezo wetu huu dhidi ya Asec na kikubwa tunazitaka pointi tatu za kila mchezo tutakaoucheza hapa nyumbani.


“Tunafahamu siyo
rahisi lakini tutapambana kufanikisha malengo yetu, uzuri timu imeingia kambini leo (jana) sambamba na kuanza mazoezi kabisa.

 

“Hivyo tumejipanga vema katika hilo, wapinzani wetu hadi kufikia leo (jana) hawajatupa taarifa za ujio
wao, hatujui sababu ni ipi,”
alisema Ally.

STORI: WILBERT MOLANDI, DAR ES SALAAM

Leave a Comment