×

Breaking: Ally Sonso Afariki Dunia

ALIYEKUWA mchezaji wa Ruvu Shooting, Ally Mtoni “Sonso” (29) amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa Matibabu leo Ijumaa, Februari 11, 2022.

Taarifa za awali zinasema kuwa, Sonso ambaye alikuwa beki wa kushoto akikuwa akiugua maradhi ya muda mrefu. Kwa nyakato tofauti, Sonso amezitumika timu za Lipuli FC, Yanga SC, Kagera Sugar, Polisi Tanzania. Pia amewahi kucheza timu ya Taifa.

Prisca Kishamba; Nasikitika kuwasilisha msiba wa Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Yanga SC na KMC FC Ally Mtoni Sonso. msiba umetokea hapa Hospital ya Taifa ya Muhimbili muda mchache uliopita. Bwana alitoa Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.

Taarifa zaidi itafuata

Apumzike kwa Amani.

James Tupatupa; Pumzika kwa Amani beki wa mpira. Ali Mtoni Sonso 🤲

Yusuph Mkule; R.I.P Ally Mtoni Sonso . Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.

Leave a Comment