
Rais Samia amesema kuanzia sasa Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi Joseph Haule (Professor Jay) anayetibiwa Muhimbili Hospitali hadi hapo atakaporuhusiwa kutoka, kauli hii imetolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alipofika Muhimbili leo.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza kuwa kuanzia sasa Serikali itagharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na Msanii Bw. Joseph Haule anayetibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi atakapo ruhusiwa kurudi nyumbani” – Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya
