×

Balozi Edwin Rutageruka Afariki Dunia

Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Edwin Rutageruka amefariki dunia jana Jumapili, Februari 13, 2022.

Familia ya Omutware Dunstan Rutageruka Musibuka imethibitisha kutokea kwa msiba huo uliotokea katika Hospital ya Agha Khan Dar es salaam jana jioni.

Balozi Rutageruka alikuwa amelazwa AghaKhan tangu juzi jioni kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua ghafla.

Rutageruka aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE)

Pumzika kwa Amani Mh. Balozi Edwin Rutageruka. Tanzania itaukumbuka Daima Mchango wako katika sekta ya Biashara, Uwekezaji na Diplomasia ya Uchumi.

Leave a Comment