×

Rais Samia Awasili Nchini Ubelgiji Leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Mhe. Charles Michel mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Baraza hilo Brussels nchini Ubelgiji leo tarehe 15 Februari, 2022.
Rais wa Samia Suluhu Hassan akiwa amewasili katika chumba cha Mkutano kwa ajili ya mazungumzo na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Mhe. Charles Michel leo tarehe 15 Februari, 2022 katika Makao Makuu ya Baraza hilo Brussels nchini Ubelgiji.

Rais Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Ubelgiji ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Baraza hilo, Brussels nchini Ubelgiji leo Februari 15 Februari, 2022.

Rais Samia yupo barani Ulaya kwa ziara ya kikazi, ambapo awali, ameitembelea Ufaransa ambapo pamoja na mambo mengine, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Emanuel Macron wan chi hiyo

Leave a Comment