Kikosi Cha 12 Cha Ulinzi Wa Amani Kutoka Tanzania Nchini DRC Chatoa Msaada Wa Matibabu Kwa Wananchi Wa Kata Ya Nzuma Beni Maviv
Kikosi cha 12 cha Ulinzi Amani kutoka Tanzania chini ya mwamvuli Monusco kimetoa huduma ya afya bure kwa wananchi wa kata ya Nzuma katika ya Mji wa beni ndani ya nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo.Huduma hiyo imetolewa ikiwa ni azma ya utekelezaji wa baadhi ya maombi yaliyotolewa na viongozi wa wananchi katika mkutano wa “URAFIKI” uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu.

Akitoa wito kwa wananchi wa Mji wa Beni mkuu wa kikosi cha 12 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania Luteni Kanali Mustafa Seif Mkundi amesema kuwa timu ya wataalamu wa afya kutoka kikosi cha 12 kimefanikiwa kutoa huduma ya matibabu kwa wazee na watoto ndani ya kata ya Nzuma na kuhaidi kuwa,kupitia mwamvuli wa Monusco wataweza kutembelea maeneo mbalimbali na kutoa huduma zitakazo weza kufanywa na walinda amani hao kutoka Tanzania.

Aidha chifu wa kata ya Nzuma Joshua Kapisa nae pia amewashukuru walinda amani kutoka Tanzania kwa kutoa msaada huo wa matibabu kwa wakazi wa kata ya Nzuma ndani ya Mji wa Beni.
Kutolewa kwa huduma hii ni muendelezo wa kuimarisha uhusiano mzuri baina ya vikundi vya ulinzi wa amani kutoka Tanzania na wananchi wa Beni Maviv katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo.


