
DROO ya mechi za kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) hatua ya robo fainali imefanyika leo Februari 21, ambapo Yanga watacheza na Geita Gold, Simba watakipiga dhidi ya Pamba, Azam na Polisi na Coastal Union wakipepertana na kagera Sugar.
Kwa mujibu wa droo hiyo mshindi kati ya mechi ya Yanga na Geita Gold, atakutana na mshindi kati ya Simba na Pamba katika hatua ya nusu fainali ya kwanza.
Mshindi kati ya Azam na Polisi atakutana na mshindi kati ya Coastal na Kagera Sugar katika hatua ya nusu fainali ya pili.