Rais Samia: Sio Tabia Yangu Kupenda Kutukuzwa – Video
Global Publishers February 22, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali wa dini katika Sherehe za kumpongeza Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi katika Jubilee ya Miaka 25 ya Utumishi wake wa Uaskofu leo tarehe 22 Februari, 2022 katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.
RAIS Samia leo Jumanne Februari 22, 2022 amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na kwamba atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.
Rais Samia amesema hayo katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.
Alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi aliyeemuomba Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.
Rais Samia akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Posta Ngara kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za kumpongeza Askofu huyo leo tarehe 22 Februari, 2022
“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine. Maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.
Sehemu ya Viongozi mbalimbali wa Dini, Mapadree, Masista, pamoja na wananchi wa Ngara wakiwa katika Jubilee ya miaka 25 ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi iliyofanyika katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.Shamrashamra za Jubilee ya Miaka 25 ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.