×

Wengine Watatu Watoweka Dar – Video

 
Vijana watatu ambao ni marafiki, Abdallah Kawambwa, Jackson Mkwetu na Omary Hamdan, wakazi wa Kitunda jijini Dar es Salaam, wamepotea katika mazingira ya kutatanisha kwa muda wa miezi mitano sasa na kuacha huzuni kubwa kwa ndugu zao ambao hawajui kilichowapata.
 
Vijana hao waliondoka majumbani kwao Septemba 10, 2021 kwa maelezo kwamba wanasafiri kuelekea mkoani Tanga lakini kuanzia hapo, hawajawahi kurudi nyumbani, simu zao hazipatikani na jitihada za ndugu zao kuwatafuta, bado hazijazaa matunda.

Leave a Comment