×

Rais Mwinyi Afunguka Watalii Wa Ukraine Waliokwama Zanzibar

Rais Mwinyi afunguka kuhusu watalii wa Ukraine waliokwama hotelini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema ni kweli kuna Watalii Raia wa Ukraine waliokwama Zanzibar baada ya Nchi yao kushambuliwa kivita na Urusi.

 

Rais Mwinyi amesema hayo leo Jumatatu, Februari 28, 2022 akiongea na wahariri wa vyombo vya Habari na wanahabari kama ilivyo kawaida yake kila mwisho wa mwezi.

 

“Taarifa nilizonazo kuna watalii wa Ukraine kama 900 tisa hivi wapo Zanzibar na hawawezi kurudi kwao, wameomba msaada ili Serikali iwasaidie hawawezi kuendelea kukaa hotelini kwa sababu hawana fedha lakini tumeanza mazungumzo wale wenye hoteli pamoja na Serikali tunazungumza kuona kwa jinsi gani tutawasaidia.
“Tunaangalia namna ya kuwasaidia mpaka Serikali yao itakapopata uwezo wa kuleta msaada kwahiyo kuna makubaliano ambayo yameanza kuonekana na Hoteli kuwapa msaada bila ya kuwachaji lakini na Serikali kuwaangalia wale wenye hoteli kwa upande wa kodi kwahiyo tunazungumza, ukweli ni kwamba tunaona umuhimu wa kutoa msaada,” amesema Rais Mwinyi.

Leave a Comment